Kitendo cha kugundulika maziwa bandia ya watoto wachanga Tanzania imedhihirika kwamba baadhi ya watu wanapofanya biashara hawana aibu wala woga wa kuangamiza maisha ya watu hata ya watoto wachanga. Mamlaka ya Chakula na dawa Tanzania (TFDA), ilikamata maziwa ya watoto wachanga aina ya NAN2 ambayo ni bandia. http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=20025 Japo Nestle wamejitetea, lakini tunajua mfanya biashara yeyote ni lazima atajitetea.  Kitendo hiki ni cha kuhatarisha maisha ya watoto na jamii.  Ni muhimu watumiaji wa maziwa haya wajifunze kutokana na tukio hili.  Baadhi ya mambo muhimu ya kufahamu ni pamoja na:

  • Namna ya kugundua lebo bandia katika maziwa au vyakula vya watoto.  Sheria inalazimu maandishi yote kuandikwa juu ya kopo na sio juu ya karatasi iliyobandikwa kwenye kopo.
  • Sheria inalazimu maandishi yote kwenye maziwa ya kopo, pamoja na lugha nyingine yoyote iliyotumika , lakini ni lazima pia yaandikwe kwa  Kiswahili.
  • Tarehe ya mwisho  ya kutumia maziwa (expiry date), lazima iwe imeandikwa kwa kuchimbwa (ingraving) kwenye kopo, na sio kuandikwa kwa wino(mhuri) au karatasi iliyobandikwa kwenye kopo. pia sio kwenye mfuniko (hii inasaidia kupunguza udanganyifu)
  • Lazima maelezo juu ya kopo yasisitize pia  jinsi Maziwa ya Mama yalivyo bora kuliko maziwa ya kopo.

Tujipende na tuwapende watoto wetu.  Pia tukumbuke Maziwa ya mama ndio bora zaidi kwa mtoto mchanga kuliko maziwa mengine yoyote. Zipo faida nyingi kwa mama na mtoto, ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa kupata saratani. http://jipende.com/archives/tag/breastfeeding/

Jipende, ufunguo wa mtindo bora wa maisha upo mkoni mwako!

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!
 Tagged as:
This entry was posted on Sunday, September 12th, 2010 at 3:26 am and is filed under Kiswahili, Lifestyle. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed. You can leave a response, or trackback from your own site.