Wapo watu wanaodhani kwamba kutumia virutubishi vya nyongeza (nutritional supplements) huweza kuzuia saratani.  Ukweli ni kwamba baada ya wataalamu kuchambua tafiti mbalimbali zilizofanyika duniani imeonekana kwamba ni bora kuepuka kutumia virutubishi vya nyongeza kwa nia ya kuzuia saratani kwani havizuii (WCRF)

Virutubishi vya nyongeza havizuii mtu kupata saratani, na pia kuna baadhi ya virutubishi ambavyo vikitumika kupita kiasi huweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani.  Ni vyema zaidi kupata virutubishi vinavyohitajika mwilini kwa kula vyakula mbali mbali vya mchanganyiko. Hakikisha unakula mboga mboga na matunda kwa wingi kila siku, nafaka hasa zile zisizong’arishwa (whole grains)  kama ulezi,  dona na mchele wa brauni, pia vyakula vya aina ya kunde.  Mafuta kiasi kidogo.  Kumbuka kumwona daktari au mtaalamu wa afya anayeelewa lishe kwa ushauri zaidi pale unapodhani kwamba una upungufu wa baadhi ya viini lishe au ukidhani unahitaji virutubishi vya nyongeza.

Jipende, usitumie virutubishi vya nyongeza bila kupata ushauri wa kitaalamu.  Tena kumbuka virutubishi vya nyongeza havizuii saratani.

Jipende, Ufunguo wa Mtindo Bora wa Maisha upo Mkononi Mwako!

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!
 Tagged as:
This entry was posted on Monday, November 8th, 2010 at 3:13 am and is filed under Kiswahili, Lifestyle. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed. You can leave a response, or trackback from your own site.