Nina hakika kila jamii ina aina ya vyakula ambavyo imevisahau au wakati mwingine wamevidharau!  Mara nyingi vyakula hivi ambavyo ni vya asili, vina ubora mkubwa.  Baadhi ya Matunda ya asili kama tunda hili kwenye picha (Kitalembo au Mtangawizi) hata jina la Kiswahili hatulijui.

Anayejua jina lake la Kiswahili atuambie ili tulitumie.  Wengi nilioongea nao kuhusu tunda hili waliniambia kwamba walilila walipokuwa watoto wadogo. Inabidi tujiulize kwa nini tunaacha kutumia matunda kama haya tunapokuwa watu wazima? Tunda hili linapatikana sehemu nyingi za Mkoa wa Kilimanjaro na naamini litakuwa pia kwenye baadhi ya Mikoa Mingine.  Majani yake yanapendwa sana na Mbuzi kwa hiyo limekuwa zaidi malisho ya mbuzi.. Naamini kukiwa na mpangilio mzuri, majani yake yanaweza kutumiwa na mbuzi lakini pia matunda yake yakaliwa na watu wote wakubwa na wadogo. Tukumbuke Matunda ya wingi wa vitamin na ni muhimu tutumie matunda kwa wingi kila siku.

Jipende.  Ufunguo wa Mtindo Bora wa Maisha Upo Mkononi Mwako…

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!
 Tagged as:
This entry was posted on Tuesday, December 20th, 2011 at 8:44 pm and is filed under Kiswahili, Lifestyle, Nutrition. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed. You can leave a response, or trackback from your own site.