Kama hunywi pombe unayo sababu ya kufurahi sana, na kwamwe usianze kunywa pombe! Kama unakunywa pombe, punguza sana, na ukiweza acha. Hii ni kwa sababu imezidi kuthibitishwa kwamba pombe ina madhara mengi kiafya.

Wataalamu waliochunguza uhusiano wa unywaji pombe na uwezekano wa kupata saratani (cancer) wamepata uthibitisho wa kuridhisha na wa uhakika kwamba unywaji pombe unaongeza uwezekano wa kupata saratani (cancer) za mdomo, koo, koromeo, matiti na utumbo mkubwa. Pia uko uthibitisho wa kiasi unahusisha unywaji pombe na uwezekano wa kupata saratani ya ini.

Unywaji pombe pia umeonekana kusababisha ongezeko la unene wa mwili na unene uliokithiri (Obesity), ambapo imethibitishwa kwamba unene huongeza uwezekano wa kupata saratani za koo, tumbo, utumbo mkubwa, matiti (baada ya “menopause”), kizazi, figo na pia uthibitisho kiasi kwa saratani ya “gall-bladder” . (chanzo-WCRF& AICR 2008).

Sasa kama mambo ya pombe ndio haya, kwa nini mtu aendelee kunywa?? Bila shaka huyo atakuwa hajipendi. Tukumbuke pia kuna uthibitisho mkubwa kwamba ulaji wa matunda na mbogo-mboga kwa wingi kila siku hupunguza uwezekano wa kupata saratani za aina nyingi. Pia mazoezi ya mwili kila siku yanapunguza uwezekano wa kupata saratani. (WCRF&AICR 2008).

Jipende! Epuka kunywa pombe. Kula matunda na mbogamboga kwa wingi kila siku, na fanya mazoezi kama vile kutembea angalau dakika 30 hadi 60 kila siku. “Ufunguo wa Mtindo Bora wa Maisha” upo mkononi mwako.

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!
 Tagged as:
This entry was posted on Sunday, March 29th, 2009 at 3:01 pm and is filed under Kiswahili, Lifestyle. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed. You can leave a response, or trackback from your own site.