Ni mchanganyiko wa: maji, sukari, rangi na ladha bandia ya matunda. Je wote tunajua hilo?  Maana ni muhimu mtua anapoamua kuvitumia vinywaji hivi afanye uamuzi huo kuzingatia taarifa sahihi alizo nazo (yaani iwe ni “informed choice”).Vinywaji hivi hata nisingependa kuviita “juisi”, maana ukweli vinywaji hivyo sio juisi.

Hivi ni vile vinywaji vya mchanganyiko wa maji, sukari, rangi na ladha bandia ya matunda (artificial fruit flavour).  Vinywaji hivi kwa kiasi kikubwa huchangia kuupa mwili nishati-lishe (calories) nyingi na isiyo na virutubishi vingine, na hivyo kuchangia ongezeko la uzito.

Zaidi ya hayo ni kwamba tunaponunua “juisi” hii bandia tunatumia fedha kwa kitu ambacho hakina faida mwilini, na pengine ni sawa kama kununua magonjwa kwani huchangia magonjwa sugu. Bei yake pia ni ndogo ukilinganisha na juisi ya kweli kwa sababu unachouziwa ni chupa iliyohifadhia, maji na sukari mara nyingi hakuna matunda kabisa au watengenezaji wengine huweka matunda kidogo sana kama aisili-mia kumi ili kutudanganya.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba watu wengi wanapoenda kuwatembelea wagonjwa huwapelekea vinywaji hivi, pengine wakidhani ni juisi.  Hata tukitembelea hospitali zetu tutaliona hilo. Tena la kusikitisha zaidi ni kwamba wapo watu wengi wanaodhani kwamba vinywaji hivyo vikiwa na rangi nyekundu au zambarau huongeza damu!! Hii sio kweli kwani vinywaji hivyo vimeongezwa tu rangi (food-colour) ambayo haina virutubishi vyovyote. Ni bora kumpelekea mgonjwa matunda au kimywaji chenye virutubishi kama maziwa.

Tena watengenezaji wanajua wazi sheria inawakataza kuviita vinywaji hivi juisi kwa hiyo wanapotumia neno juisi wengine hubadili “spelling” kidogo, kwa kiasi ambacho sisi walaji hatutambui kwa urahisi. Wengine wanafuata sheria za nchi na za kimataifa ambapo wakiongeza neno “Drink” sheria inamlinda, Kwa maana hiyo kinywaji kilichoandikwa  “juice Drink” sio juisi halisi ya matunda. (sio 100% Juice), juisi halisi siku zote huandikwa “100% juice”. Ni muhimu kusoma lebo, lakini nadhani kwa bahati mbaya watumiaji wengi hawana taarifa ya namna sahihi ya kusoma lebo.  Tumia zaidi matunda au juisi halisi ya matunda.

Siku ingine nitatoa vidokezo vya namana ya kusoma lebo ya vyakula.  Endelea kutembelea blogu hii.

Jipende! Ufunguo wa mtindo bora wa maisha upo mkononi mwako

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!
 Tagged as:
This entry was posted on Saturday, July 4th, 2009 at 4:20 am and is filed under Kiswahili, Lifestyle, Nutrition. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed. You can leave a response, or trackback from your own site.