Posts Tagged with ‘sukari’
Posted by Mary G. Materu Msc
Today’s Tip: Be smart..
- Balance your calorie intake with your physical activity
- If you are overweight or obese, work hard to reduce your weight and stay at healthy weight
This is just a reminder: Remember, being overweight increases your risk of many types of cancers eg. breast and colon cancers. Control your weight by making sure you burn more calories than those you eat. Watch the portion size of the meals that you eat.. Go for small portion size, add more vegetables into your meals, avoid foods high in fat and high in sugar, limit or avoid alcohol intake, add exercise eg. working into your routine life.
Jipende: Ufunguo wa Mtindo Bora wa Maisha upo Mkononi Mwako…
Posted by Mary G. Materu Msc
Sehemu ya pili
Ugonjwa wa moyo (coronary heart disese) una dalili kadhaa lakini mojawapo ni moyo kushindwa kazi (heart attack). Tatizo hili la moyo kushindwa kazi hutokea ghafla na hasa kwa watu wenye umri mkubwa lakini ukweli ni kwamba ugonjwa huo unakuwa umeanza muda mrefu uliopita, pengine miaka mingi iliyopita. Ndio maana ni muhimu kuanza kuutunza moyo mapema wakati wa ujana hata utotoni.
Naamini ulisoma sehemu ya kwanza kwa hiyo hapa tunaendelea na sehemu ya pili kwa kuzungumzia shinikizo kubwa la damu (high blood pressure) na ugonjwa wa kisukari kwani magonjwa haya pia huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo.
Shinikizo kubwa la damu (high blood Pressure) huharibu ngozi ya ndani ya mishipa ya damu na hivyo kufanya lehemu (Cholesterol) kujikusanya kwenye mishipa ya damu kwa urahisi zaidi. Punguza uwezekano wa kuwa na shinikizo kubwa la damu kwa kufanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku, kuwa na uzito wa mwili usiozidi kiasi na kupunguza matumizi ya chumvi na vyakula vyenye chumvi nyingi. Kama tayari una shinikizo kubwa la damu, endelea kutumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari wako na kufuata ushauri wa chakula na lishe. Kumbuka ni muhimu sana kutumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari.
Kuwa na ugonjwa wa kisukari pia huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo. Kwa bahati mbaya, watu wengi wenye ugonjwa wa kisukari hata hawajui kwamba wana ugonjwa huo. Ugonjwa wa kisukari huweza kuharibu mishipa ya damu, na hii inaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo. Pia ugonjwa wa kisukari huongezea uwezekano wa kuwa lehemu nyingi mwilini, kupata shinikizo kubwa la damu na pia kuwa na unene kupita kiasi. Kipimo cha damu kuona kiasi cha sukari katika damu hugundua kama una ugonjwa wa kisukari au una uwezekano wa kupata kisukari. Hivyo ni muhimu kumwona mtalamu wa afya kupata huduma hiyo ya kupima damu. Kama tayari una ugonjwa wa kisukari basi ni muhimu kuendelea kufuatilia huduma za afya ili uelekezwe ulaji bora unasaidia kuuweka mwili katika kiasi cha wastani cha sukari au kupatiwa dawa pale inapohitajika. Punguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari kwa kuhakikisha huna uzito uliozidi kiasi, kufanya mazoezi ya mwili kila siku angalau dakika 30 au zaidi, kupunguza matumizi ya mafuta au vyakula vyenye mafuta mengi, pia vile vyenye sukari nyingi kwani huchangia kuongeza uzito.
Mpaka sasa naamini umegundua kwamba kutokufanya mazoezi ya mwili kunaongeza uwezekano wa kupata magonjwa sugu mengi, na pia ikiwepo ugonjwa wa moyo. Kufanya Mazoezi ya mwili itakupunguzia uwezekano wa kupata magonjwa haya sugu. Chagua zoezi ambalo unamudu. Kwa mfano kutembea kwa haraka kwa angalau dakika 30 kwa siku na ukishazoea ongeza kufikia angalau saa moja (dakika 60). Kama unafanya kazi au kuishi gorofani tumia ngazi badala ya lifti; fanya kazi za nyuimbani kama kusafisha, kufua, kupasi bustani nk. kama sehemu ya mazoezi. Punguza muda unaoketi kuangalia TV, na epuka vyakula vinavyo ongeza uzito kwa haraka kama vile vyenye mafuta mengi au sukari nyingi. Pia kula chakula kwa kiasi, huku ukihakikisha unatumia mbogamboga kwa wingi, matunda na nafaka zisizong’arishwa kama dona.
Yapo mengi unayoweza kufanya kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo, lakini sio lazima uanze yote kwa mara moja. Anza kidogo kidogo mwisho utakuta umeweza yote. Kila unapopiga hatua moja ni mchango mkubwa kwa maisha yako. Jiwekee malengo na taratibu za kukusaidia kutimiza malengo yako. Kwa mfano weka rekodi ya dakika ulizofanya mazoezi kwa siku na ichunguze rekodi hiyo kila mwisho wa wiki ili uweze kuongeza bidii. Kama una mtindo wa kula asusa (snacks) zenye mafuta mengi au sukari nyingi, jiwekee karibu nawe asusa zisizo na mafuta kama karoti, tunda, tango, mahindi ya kuchoma au kukaanga (popcorn), maji na kadhalika.
Ukweli ni kwamba unaweza!!! Lenga mabadiliko katika namna unavyokula, ongeza mazoezi ya mwili na epuka utumiaji wa sigara au tumbaku.
Jipende…. Ufunguo wa mtindo bora wa maisha upo mkoni mwako.
Posted by Mary G. Materu Msc
Wakati asali hulitumika sio tu kama chakula bali baadhi ya watu huitumia pia kama dawa, wengine wameona ndio mwanya wa kutafuta faida ya haraka bila hata woga kwamba wanaangamiza maisha ya watu wengine. Baadhi ya asali inayouzwa kwenye barabara za Dar es Salaam imechanganywa na maji na sukari guru! Hii huwafanya waweze kuuza asali hiyo bandia kwa bei nafuu sana, lakini ukweli ni kwamba hiyo sio asali tena. Hii ilidhihirika zaidi siku moja ambapo rafiki yangu aliyenunua asali barabarani, akatoa shilingi elfu 5, muuzaji alimwambia ngoja akatafute chenji, akamwachia chupa nyingi za asali, lakini alitokomea bila kurudi wala kujali asali alizoziacha. Ndipo ikagundulika kwamba ilikuwa asali bandia. Kwanza licha ya asali hiyo kuwa bandia, chupa zinazotumika ni ambazo watu wamemaliza kunywa maji au chupa za konyagi, na huenda hazikusafishwa vizuri.

Epuka asali isiyo na viwango
Nyuki hutengeneza asali kutokana na nta wanayokusanya kutoka maua mbalimbali. Nyuki hutegemea asali hiyo kama chakula chao hasa wakati ambapo sio msimu wa maua kuchanua. Asali iliyokomaa kwa kawaida ina kiasi kidogo cha maji, chini ya asilimia ishirini (20%). Asali pia ina viini-lishe mbalimbali kwa kiasi kidogo, ikiwa ni pamoja na vitamin, madini na protini. Kilichopo kwa wingi katika asali ni sukari ambayo ni asilimia themanini (80%). (angalia viwango vya asali-codex). Kutokana na asali kuwa na sukari nyingi, ina maana kama ilivyo sukari, asali ikitumika kwa wingi, humwongezea mtu uzito, kwa sababu ina nishati-lishe nyingi.
Tangu asili, ni kwamba asali ilikuwa ni kitu maalumu sana ambacho mtu hutumia kiasi kidogo tu, kwa hiyo hatari ya kumwongezea mtu uzito haikuwepo. Mara nyingi mtu anayetuamia asali alikuwa anatumia kijiko kimoja au viwili kwa siku na sio kila siku!
Sasa tukirudi kwenye tatizo la wanaochanganya maji kwenye asali wanayouza na matatizo yake, sio kwamba tu wanaweza kutumia maji yaliyo machafu, bali pia ni wadanganyifu na wanaiharibu asali. Asali inapokuwa na maji zaidi ya asilimia ishirini (20%), inachacha mapema (inaharibika) na inaota ukungu (fangus). Kumbuka ukungu kwenye chakula hauonekani kwa macho mapema, mpaka unapoonekana ni kwamba ulishaota siku nyingi! Kwa kawaida asali iliyokomaa na isiyochanganywa maji na ikihifadhiwa vizuri haiharibiki kwa miaka mingi, bila hata kuwekwa kwenye jokofu (refrigerator).
Kiasi cha maji katika asali hupimwa kwa chimbo kinachoitwa “honey refractometer”, (naamini wasimamiaji wa ubora wa asali ndio wenye chombo hiki). Katika kuweka viwango vya asali zipo nchi nyingine ambazo zimeweka kiwango cha maji kinachoruhusiwa katika asali chini kwao kuwa cha chini zaidi ili kuongeza ubora, kwa mfano Marekani wameweka kiwango cha asilimia kumi na nane na nusu (18.5%), ambapo kiwango cha kimataifa kilichowekwa na “Codex alimentarius” (FAO/WHO) ni kwamba maji kwenye asali yasizidi asilimia ishirini (20%). Sasa sisi hapa Tanzania nani atatulinda?? Ukweli ni kwamba tunawategemea Shirika la viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuweka sheria kali pamoja na ufuatiliaji. Tunaamini mashirika yetu haya mawili pamoja na wadau wengine wanaweza kuthibiti ubora wa asali Tanzania ili kuokoa maisha ya watu.
Nadhani pia kwa wanunuzi wa asali itabidi kuwa waangalifu, labda kuepuka kabisa asali zinazouzwa kiholela bila nembo ya TBS. Tuwe macho tusikubali kudanganywa!!
Jipende… Ufungunguo wa mtindo bora wa maisha upo mkononi mwako.