login/logout

Posts Tagged with ‘viwango’

Posted by Mary G. Materu Msc

Wakati asali hulitumika sio tu kama chakula bali baadhi ya watu huitumia pia kama dawa, wengine wameona ndio mwanya wa kutafuta faida ya haraka bila hata woga kwamba wanaangamiza maisha ya watu wengine.  Baadhi ya asali inayouzwa kwenye barabara za Dar es Salaam imechanganywa na maji na sukari guru!  Hii huwafanya waweze kuuza asali hiyo bandia kwa bei nafuu sana, lakini ukweli ni kwamba hiyo sio asali tena.  Hii ilidhihirika zaidi siku moja ambapo rafiki yangu aliyenunua asali barabarani, akatoa shilingi elfu 5, muuzaji alimwambia ngoja akatafute chenji, akamwachia chupa nyingi za asali, lakini alitokomea bila kurudi wala kujali asali alizoziacha. Ndipo ikagundulika kwamba ilikuwa asali bandia.  Kwanza licha ya asali hiyo kuwa bandia, chupa zinazotumika ni ambazo watu wamemaliza kunywa maji au chupa za konyagi, na huenda hazikusafishwa vizuri.

Epuka asali isiyo na viwango

Nyuki hutengeneza asali kutokana na nta wanayokusanya kutoka maua mbalimbali.  Nyuki hutegemea asali hiyo kama chakula chao hasa wakati ambapo sio msimu wa maua kuchanua.  Asali iliyokomaa kwa kawaida ina kiasi kidogo cha maji, chini ya asilimia ishirini (20%).   Asali pia ina viini-lishe mbalimbali kwa kiasi kidogo, ikiwa ni pamoja na vitamin, madini na protini.  Kilichopo kwa wingi katika asali ni sukari ambayo ni asilimia themanini (80%).  (angalia viwango vya asali-codex).  Kutokana na asali kuwa na sukari nyingi, ina  maana kama ilivyo sukari, asali ikitumika kwa wingi, humwongezea mtu uzito, kwa sababu ina nishati-lishe nyingi.

Tangu asili, ni kwamba asali ilikuwa ni kitu maalumu sana ambacho mtu hutumia kiasi kidogo tu, kwa hiyo hatari ya kumwongezea mtu uzito haikuwepo. Mara nyingi mtu anayetuamia asali alikuwa anatumia kijiko kimoja au viwili kwa siku na sio kila siku!

Sasa tukirudi kwenye tatizo la wanaochanganya maji kwenye asali wanayouza na matatizo yake, sio kwamba tu wanaweza kutumia maji yaliyo machafu, bali pia ni wadanganyifu na wanaiharibu asali.  Asali inapokuwa na maji zaidi ya asilimia ishirini (20%), inachacha mapema (inaharibika) na inaota ukungu (fangus). Kumbuka ukungu kwenye chakula hauonekani kwa macho mapema, mpaka unapoonekana ni kwamba ulishaota siku nyingi! Kwa kawaida asali iliyokomaa na isiyochanganywa maji na ikihifadhiwa vizuri haiharibiki kwa miaka mingi, bila hata kuwekwa kwenye jokofu (refrigerator).

Kiasi cha maji katika asali hupimwa kwa chimbo kinachoitwa “honey refractometer”, (naamini wasimamiaji wa ubora wa asali ndio wenye chombo hiki).  Katika kuweka viwango vya asali zipo nchi nyingine ambazo zimeweka kiwango cha maji kinachoruhusiwa katika asali chini kwao  kuwa cha chini zaidi ili kuongeza ubora, kwa mfano Marekani wameweka kiwango cha asilimia kumi na nane na nusu (18.5%), ambapo kiwango cha kimataifa kilichowekwa na “Codex alimentarius” (FAO/WHO) ni kwamba maji kwenye asali yasizidi asilimia ishirini (20%).  Sasa sisi hapa Tanzania nani atatulinda?? Ukweli ni kwamba tunawategemea Shirika la viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuweka sheria kali pamoja na ufuatiliaji.  Tunaamini mashirika yetu haya mawili pamoja na wadau wengine wanaweza kuthibiti ubora wa asali Tanzania ili kuokoa maisha ya watu.

Nadhani pia kwa wanunuzi wa asali itabidi kuwa waangalifu, labda kuepuka kabisa asali zinazouzwa kiholela bila nembo ya TBS. Tuwe macho tusikubali kudanganywa!!

Jipende… Ufungunguo wa mtindo bora wa maisha upo mkononi mwako.

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!
Posted by Mary G. Materu Msc

Bread

When we ask for a brown bread at a shop what are we asking for? Is it just the colour of the bread? If it is just the colour, then we could have added any edible colour to make a white bread brown! No doubt when we ask for a brown bread we are asking for a ‘whole wheat bread’ not just brown coloured bread. Unfortunately, in Tanzania most bakers do not label or do not adequately label the bread.

(more…)

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!

All Right Reserved, Copyright © 2009 - 2010 Jipende.com
Designed by Qualtek Ventures