Katika matunda yenye vitamin C kwa wingi, ubuyu ni mojawapo. Tunda hili pamoja na virutubishi vingine, lina vitamin C kwa wingi sana lakini hata pale tunda hili linapopatikana halitumiki ya kutosha. Tunapozungumzia “kula matunda kwa wingi kila siku”, ubuyu unaweza kuwa sehemu ya matunda hayo. Pia ubuyu unaweza kutumika kutengeneza kinywaji kwa kutumia unga wake kuchanganya na maji yaliyo safi na salama. Ubuyu pia unaweza kuchanganywa kwenye uji ambapo unaongeza ladha na virutubishi hasa vitamin C.







