Zambarau (Jambolan fruit) ni tunda moja zuri lakini mara nyingi linasahaulika au kudharauliwa. Kama matunda mengine mengi, tunda hili lina wingi wa vitamini C, pia vitamini nyingine ikiwepo A. Tukumbuke kwamba kila tunapoweza kuchanganya vyakula vya rangi mbali mbali katika mlo tunayotumia, basi tunaongeza ubora. Ongeza rangi ya zambarau katika matunda unayotumi, iwapo zinapatikana pale unapoishi. Hasa wakati wa msimu wake.
Archive for May, 2010
Usafi na usalama wa chakula ni muhimu kwa kila mtu japo hapa namlenga zaidi mgonjwa wa saratani. Hii ni kwa sababu kinga ya mwili ya mgonjwa wa saratani imepungua kutokana na ugonjwa, kwa hiyo lazima ajitahidi sana kuzingatia usafi na usalama wa chakula. Pamoja na kutimiza kanuni zote za usafi wa mikono, vyombo, mazingira na maji ya kunywa, ni muhimu kuwa mwangalifu sana wakati tunapotayarisha au kutumia vile vyakula ambavyo kwa kawaida vina hatari kubwa zaidi ya maambukizi hasa ya magonjwa (hasa “salmonella”). Vyakula hivyo ni nyama yoyote mbichi (ikiwepo nyama ya kuku), mayai mabichi na samaki wabichi.






