Zambarau (Jambolan fruit) ni tunda moja zuri lakini mara nyingi linasahaulika au kudharauliwa. Kama matunda mengine mengi, tunda hili lina wingi wa vitamini C, pia vitamini nyingine ikiwepo A. Tukumbuke kwamba kila tunapoweza kuchanganya vyakula vya rangi mbali mbali katika mlo tunayotumia, basi tunaongeza ubora. Ongeza rangi ya zambarau katika matunda unayotumi, iwapo zinapatikana pale unapoishi. Hasa wakati wa msimu wake.
Archive for the ‘Lifestyle’ Category
Usafi na usalama wa chakula ni muhimu kwa kila mtu japo hapa namlenga zaidi mgonjwa wa saratani. Hii ni kwa sababu kinga ya mwili ya mgonjwa wa saratani imepungua kutokana na ugonjwa, kwa hiyo lazima ajitahidi sana kuzingatia usafi na usalama wa chakula. Pamoja na kutimiza kanuni zote za usafi wa mikono, vyombo, mazingira na maji ya kunywa, ni muhimu kuwa mwangalifu sana wakati tunapotayarisha au kutumia vile vyakula ambavyo kwa kawaida vina hatari kubwa zaidi ya maambukizi hasa ya magonjwa (hasa “salmonella”). Vyakula hivyo ni nyama yoyote mbichi (ikiwepo nyama ya kuku), mayai mabichi na samaki wabichi.
Katika matunda yenye vitamin C kwa wingi, ubuyu ni mojawapo. Tunda hili pamoja na virutubishi vingine, lina vitamin C kwa wingi sana lakini hata pale tunda hili linapopatikana halitumiki ya kutosha. Tunapozungumzia “kula matunda kwa wingi kila siku”, ubuyu unaweza kuwa sehemu ya matunda hayo. Pia ubuyu unaweza kutumika kutengeneza kinywaji kwa kutumia unga wake kuchanganya na maji yaliyo safi na salama. Ubuyu pia unaweza kuchanganywa kwenye uji ambapo unaongeza ladha na virutubishi hasa vitamin C.

Baadhi ya vyakula vya asili hata majina ya Kiswahili hatuyajui, au niseme mimi siyajui. Viazi vikuu ni baadhi ya vyakula ambavyo wengi wameacha kabisa kuvitumi, na pengine vijana wengi na watoto hawajaviona kabisa. Kiazi kimojawapo, jamii ya viazi vikuu, ambacho mimi sijui jina lake la Kiswahili ni hiki kwenye picha hii:

Mkoani Kilimanjaro wapo wanaokiita “Nduu”. Na wengine hukiita “Mamaya”, yapo makabila Tanzania wanayoviita “Vibere”
Kiazi hiki huzaa viazi kwenye matawi yake ambayo hutambaa juu ya mti na pia huzaa viazi katika mizizi yake. Vyote vina ladha nzuri.






