Kama hunywi pombe unayo sababu ya kufurahi sana, na kwamwe usianze kunywa pombe! Kama unakunywa pombe, punguza sana, na ukiweza acha. Hii ni kwa sababu imezidi kuthibitishwa kwamba pombe ina madhara mengi kiafya.
Wataalamu waliochunguza uhusiano wa unywaji pombe na uwezekano wa kupata saratani (cancer) wamepata uthibitisho wa kuridhisha na wa uhakika kwamba unywaji pombe unaongeza uwezekano wa kupata saratani (cancer) za mdomo, koo, koromeo, matiti na utumbo mkubwa. Pia uko uthibitisho wa kiasi unahusisha unywaji pombe na uwezekano wa kupata saratani ya ini.






