Posts Tagged with ‘Nutrition’
Posted by Mary G. Materu, (Msc)
Kama ambavyo nimewahi kusema hapo awali, baadhi ya vyakula vya asili ambavyo pia vina virutubishi (viini-lishe) vingi na pengine gharama kidogo vinasahaulika au kudharauliwa. Leo nazungumzia nyanya-mti (wengine huliita “matungusha”).

Nyanya-mti
Tanzania tunda hili linapatikana sana mkoa wa Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya na mingineyo. (more…)
Posted by Mary G. Materu, (Msc)
Zambarau (Jambolan fruit) ni tunda moja zuri lakini mara nyingi linasahaulika au kudharauliwa. Kama matunda mengine mengi, tunda hili lina wingi wa vitamini C, pia vitamini nyingine ikiwepo A. Tukumbuke kwamba kila tunapoweza kuchanganya vyakula vya rangi mbali mbali katika mlo tunayotumia, basi tunaongeza ubora. Ongeza rangi ya zambarau katika matunda unayotumi, iwapo zinapatikana pale unapoishi. Hasa wakati wa msimu wake.
(more…)
Posted by Mary G. Materu, (Msc)
Usafi na usalama wa chakula ni muhimu kwa kila mtu japo hapa namlenga zaidi mgonjwa wa saratani. Hii ni kwa sababu kinga ya mwili ya mgonjwa wa saratani imepungua kutokana na ugonjwa, kwa hiyo lazima ajitahidi sana kuzingatia usafi na usalama wa chakula. Pamoja na kutimiza kanuni zote za usafi wa mikono, vyombo, mazingira na maji ya kunywa, ni muhimu kuwa mwangalifu sana wakati tunapotayarisha au kutumia vile vyakula ambavyo kwa kawaida vina hatari kubwa zaidi ya maambukizi hasa ya magonjwa (hasa “salmonella”). Vyakula hivyo ni nyama yoyote mbichi (ikiwepo nyama ya kuku), mayai mabichi na samaki wabichi. (more…)
Posted by Mary G. Materu, (Msc)
Katika matunda yenye vitamin C kwa wingi, ubuyu ni mojawapo. Tunda hili pamoja na virutubishi vingine, lina vitamin C kwa wingi sana lakini hata pale tunda hili linapopatikana halitumiki ya kutosha. Tunapozungumzia “kula matunda kwa wingi kila siku”, ubuyu unaweza kuwa sehemu ya matunda hayo. Pia ubuyu unaweza kutumika kutengeneza kinywaji kwa kutumia unga wake kuchanganya na maji yaliyo safi na salama. Ubuyu pia unaweza kuchanganywa kwenye uji ambapo unaongeza ladha na virutubishi hasa vitamin C.

(more…)