Zambarau (Jambolan fruit) ni tunda moja zuri lakini mara nyingi linasahaulika au kudharauliwa. Kama matunda mengine mengi, tunda hili lina wingi wa vitamini C, pia vitamini nyingine ikiwepo A. Tukumbuke kwamba kila tunapoweza kuchanganya vyakula vya rangi mbali mbali katika mlo tunayotumia, basi tunaongeza ubora. Ongeza rangi ya zambarau katika matunda unayotumi, iwapo zinapatikana pale unapoishi. Hasa wakati wa msimu wake.
Posts Tagged with ‘Saratani’
Usafi na usalama wa chakula ni muhimu kwa kila mtu japo hapa namlenga zaidi mgonjwa wa saratani. Hii ni kwa sababu kinga ya mwili ya mgonjwa wa saratani imepungua kutokana na ugonjwa, kwa hiyo lazima ajitahidi sana kuzingatia usafi na usalama wa chakula. Pamoja na kutimiza kanuni zote za usafi wa mikono, vyombo, mazingira na maji ya kunywa, ni muhimu kuwa mwangalifu sana wakati tunapotayarisha au kutumia vile vyakula ambavyo kwa kawaida vina hatari kubwa zaidi ya maambukizi hasa ya magonjwa (hasa “salmonella”). Vyakula hivyo ni nyama yoyote mbichi (ikiwepo nyama ya kuku), mayai mabichi na samaki wabichi.
Kutokana na tafiti nyingi zilizofanyika, wataalamu wameona kwamba kitendo cha mama kumnyonyesha mtoto kwa matiti yake huchangia katika kupunguza uwezekano wa mama kupata saratani (cancer) ya matiti. (World Cancer Research Fund; http://www.wcrf.org/). Imeonekana kwamba sasa kuna uthibitisho mkubwa kuhusu jambo hili.
Nafaka zisizokobolewa (whole grains), aina mbali mbali za kunde na maharage (legumes) zimeonekana kuupa mwili afya bora na faida nyingi sana ikiwepo kuzuia baadhi ya saratani (cancer). Tujizoeshe kula na tufurahie kula vyakula hivi. Nafaka zisizokobolewa ni kama unga wa dona, mkate wa brauni (uliotengenezwa na ngano ambayo haikukobolewa sana), mchele wa brauni na ulezi, pia mtama (sorghum) au uwele ambao haukukobolewa. Jamii za mikunde zinahusisha maharage, kunde, mbaazi, njugu mawe, choroko, fiwi, dengu, njegee kavu nk.






