Zambarau (Jambolan fruit) ni tunda moja zuri lakini mara nyingi linasahaulika au kudharauliwa.  Kama matunda mengine mengi, tunda hili lina wingi wa vitamini C, pia vitamini nyingine ikiwepo A.  Tukumbuke  kwamba kila tunapoweza kuchanganya vyakula vya rangi mbali mbali katika mlo tunayotumia, basi tunaongeza ubora.  Ongeza rangi ya zambarau katika matunda unayotumi, iwapo zinapatikana pale unapoishi.  Hasa wakati  wa msimu wake.

Uzuri wa kununua matunda wakati wa msimu wake ni kwamba mara nyingi yatakuwa freshi na bei itakuwa nafuu.  Wakati wa msimu wa zambarau hata Jijini Dar es Salaam tunda hili huwa na bei nafuu.  Cha kushangaza ni kwamba zinauzwa zaidi katikati ya jiji tu!! Tujiulize kwa nini hazifiki kwenye magenge yetu kule tunakoishi, au kwa nini hazitembezwi pia kule tunapoishi( isipokuwa katikati ya jiji)?   je sisi wengine tunazidharu zambarau? Tulitumie tunda hili pale linapipatikana, tulithamini, tulipende!

Kumbuka: Tumia matunda na mbogamboga kwa wingi kila siku!  Punguza uwezekano wa kupata saratani na magonjwa mengine.

Jipende: Ufunguo wa mtindo bora wa maisha upo mkononi mwako

SANY0333 (1000 x 750)

del.icio.us Digg Facebook Google Twitter Mail to a friend Thank you for sharing!
 Tagged as:
This entry was posted on Saturday, May 29th, 2010 at 1:39 am and is filed under Kiswahili, Lifestyle, Nutrition. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed. Both comments and pings are currently closed.